NOVENA MT. RITAKASHIA SIKU YA PILI
NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA SIKU YA PILI
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina
Ewe mfanya miujiza Mtakatifu Rita wa Kashia. Naona njia ya maisha yako imejaa majaribu na miiba
mingi inayochoma, ambayo nahofia imepasua moyo wako vipande vipande. Ee Rita uliye kweli
shahidi wa maumivu makali. Uliyeonja tone kwa tone, hadi ukamaliza kikombe chote cha maumivu
makali. Nafikiria juu ya moyo wako uliochoka kabisa. Ninakugeukia na kumwomba Mungu kwa
maombezi yako
(Ee mwenyezi Mungu kwa maombezi ya Mt Rita wa kashia tunaendelea kukuomba uwaponye wagonjwa wote wenye ugonjwa wa Corona na utukinge na ugonjwa huu utujalie Afya njema katika Taifa letu na Dunia nzima)unaweza kuongeza ombi lako)
Wewe unajua maana ya moyo unaovuja damu. Unajua pia kifo dini cha roho. Umeumizwa sana na
kuteseka sana. Kwa njia ya mateso hayo nakuomba unisaidie katika mahangaiko yangu. Je, si kweli
kwamba wakati huu mgumu, Bwana wetu Yesu ametuandalia njia ya kujipatia neema; kupitia
miujiza ambayo binadamu wanaweza kukuomba kwa matumaini na kwa maombezi yako
wakafanikiwa?
Ee Mtakatifu mpenzi, iangalie roho iliyopondeka inayolia na kuhuzunika mbele yako.
Ninakutumainia, Ee Mtakatifu Rita. Niombee kwa Yesu mbinguni ili nipate kupokea yote
ninayomwomba Mungu kwa maombezi yako yenye nguvu.
Baba yetu ×3
Salamu Maria ×3 Atukuzwe Baba ×3
♢ Kwa njia ya Mtakatifu Rita: - homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na
ghadhabu vitoweke.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
♢ Kwa maombezi yako:-radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego
yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
♢Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba
sifa zako. Kashia hutukusa jina lako.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
♢Kwa Mungu Mtakatifu na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za
pendo la milele.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi: Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
Tuombe: Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali
kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso.
Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya
mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele Amina.
Comments
Post a Comment