SIKU YA SABA: NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

SIKU YA SABA(7)

 NOVENA YA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA

Kwa jina LA Baba, nala Mwana, nala Roho Mtakatifu . AMINA*.

Ee mpedwa Rita, ambaye maisha yako yalikuwa yahuzuni. Nielekezee uso wako wa huruma mimi mwenye maumivu makali. Naomba sala zangu, uchovu wangu na kuchechemea kwangu viufikie moyo wako mpole ili uweze kufunguliwa kwangu. Huruma yako ambayo wakati wote uliionesha kwa Jiran, maneno ya aman na faraja, na ushauri Mtakatifu uliowapa watu wote vinivute kukuelekea wewe uliye katika mbingu na unakoishi na kuwa mwombezi wa watu wote waliokata tamaa.
Mbele ya miujiza yako mikuu, kifo kinarudi nyuma, vipofu wanapokea nuru, viwete wanasimama, waliopooza wanaponyeshwa na ulemavu wote wa roho na mwili unaondoka kabisa. Je! Nipo peke yangunjsiyefarijiwa na maombezi yako? Sitaamini wala siwezi kuamin hivyo. Nam naamini kwa dhati usimamizi wako na maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ninamatumaini makubwa kuwa nitapata amani, moyoni wang, utulivwana fadhila ninazoomba nitajaliwa, [ HAPA OMBA HITAJI LAKO UNALOTAKA KUMWOMBA MUNGU KUPITIA MTAKATIFU RITA]
Baba yetu×3, Salam Maria×3, na Atukuzwe Baba×3
¶Kwa njia ya Mtakatifu Rita~ homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
¶Kwa maombezi yako~ radio, tetemeko LA ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari na vitisho vyote hutoweka.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete ; watoto wanaomba sana na watu unawarudishia uhai.
¶ Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo wa mambo yaliyoshindikana, watu wengi wanaimba sifa zako Kashia hutukuza jina lako;
Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi, watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
¶ Kwa Mungu Mtakatifu, nakwa mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete , watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
KIONGOZI: Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako RITHA.
WOTE: Kwa muhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE; Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohon mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yako, neema za kusamehee adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa Wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele . AMINA
Litania...........
*NOVENA YA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA -SIKU YA NANE*.(😎
*Kwa jina la Baba,na la Mwana, na la Roho Mt. Amina*
Ewe kielelezo kitakatifu cha Msalaba Mtukufu, ninapokuona ukiwa umesujudu mbele ya miguu mitakatifu ya Bwana,ninapotafakari paji la uso wako lililojeruhiwa kwa mwiba uliotoka ktk taji la miiba la Yesu Kristo, mchumbawako mpendwa, imani yangu kwako inachanua kwa namna ya ajabu. Wewe ni mtumishi mteule wa Mungu. Mungu amekuzawadia alama ya ufalme wake akakutakatifuza na kukufanya uwe mali yake kabisa.
Hivyo sikukosea nilivyoweka imani yangu yote kwako,na nilipojiweka kabisa chini ya ulinzi wako wenye huruma nyingi. Na sasa ni wakati mzuri wa kunisaidia, ukiyajua mahitaji na misaada ninayoomba kutoka kwako. Naamini sala hii kwako wewe mama mpenz sana haitapotea bure.
Wew uliye mfanya miujiza, mfadhili wa mambo ya mbinguni, unayetegemewa na wanadamu wote. Ninakuomba na kukusihi kwa mastahili ya pendo lako kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, uniombee ili nijaliwe haya niombayo( *hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Ritha*. )
Mungu hakukatalii wew kitu chochote; kwa maombezi yako,miujiza hufanywa,neema na fadhila maalumu hupatikana. Hivyo, kwa moyo wangu wote na matumaini ya dhati,ninasubiri nikitegemea kupata haya niliyoomba kwa Bwana Mungu.
*Baba Yetu x3, Salamu Maria x3 na Akukuzwe Baba x3*
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke .
*Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete:- watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako: radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka_ .
*Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete:- watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako
*Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi:- watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele.
*Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete:- watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.*
*KIONGOZI* : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Ritha.
*WOTE:* Kwa muhuri wa upendo na mateso.
*TUOMBE;* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele . AMINA
LITANIA........
*NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA SIKU YA TISA (9)*
*Kwajina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*
Nina kuja mbele yako, Ee Mtakatifu Rita, siku hii ya mwisho ya Novena hii Takatifu. Ninayasikia mapigo ya moyo katika kipindi hiki kigumu cha maisha yangu yaliyogawanyika. Ninaamini kwamba ombi langu litatimizwa na Bwana kupitia maombezi yako Matakatifu. Lakini ikiwa haiwezekani,ninapaza sauti nikiomba kwanguvu huruma na faraja yako. Usiniache niondoke bila kupata faraja yako.
Ee Mtakatifu Rita ,ninaomba unifariji kwa mastahili ya mateso uliyoyapata hapa duniani na katika upweke wako wa sala. Unifariji kwa mastahili ya ukarimu uliokua nao kwa wenye shida unisikilize kwa kwa mastahili ya upendo wako mkuu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa mama yake Bikira Maria Mtakatifu asiye na doa. Kwa mastahili ya ule mwiba Mtakatifu aliokujalia Bwana wetu Yesu Kristo,unisaidie na unifadhili mimi.
Hiki ndicho kilio changu cha mwisho kwako wewe mama uliye Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa. Ninakuomba ujidhihirishe katika mwanga wako halisi, ili Mungu anijalie haya ninayo yaomba.
*(hapa omba hitaji lako unalotaka kumuomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita)*
Kwa msaada wako ninadhamiria kuachana na mwenendo wangu potofu, ili niwe muenezaji wa nguvu za Mungu na uzuri wa mambo ya Mbinguni. Ninaahidi pia mahali pako pa upweke, Ee Mtakatifu wa sala,huko Kashia,na au kwenye sanamu yako: ili niweze kuungana nawe katika kuabudu na kushukuru kwa fadhila za Mbinguni nilizozipata kwa maombezi yako kutoka kwa Mwokozi wetu Azizi Yesu Kristo.
*Baba Yetu 3, Salamu Maria 3, Atukuzwe 3*
🛐Kwa njia ya Mtakatifu Rita : homa, madonda na tauni,viini vya maradhi mbalimbali na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai*.
🛐Kwa maombezi yako: radi,tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. *Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete :watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai*.
🛐Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mabo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako.Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai*.
🛐Kwa Mungu Mtakatifu na kwa mwanae ziwe sifa,utukufu na heshima,sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai*
*KIONGOZI* : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
*WOTE* :Kwa mhuri wa upendo na mateso.
*TUOMBE* : Ee Mungu,uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka . Unayeishi na kutawala, daima na milele. *Amina*
Litania ya Mt Rita wa Kashia

Comments

Popular posts from this blog

SIKU NANE: NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA