NOVENA YA EKARISTI TAKATIFU
NOVENA YA EKARISTI TAKATIFU(Mwili na Damu) Katika Ekaristi Takatifu fumbo la Ukombozi wetu linawekwa hai na kufikia kilele katika sadaka ya Bwana: “huu ndio Mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu na hii ndiyo Damu yangu itakayomwagika kwa ajili yenu”, “Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi” (Luka 22:19-20). Sisi sote tunaalikwa kwenye karamu hii ili tuweze kushiriki katika uzima ule ule wa Kristo Yesu! (NJOO KWANGU) INAPATIKANA KTK KITABU CHA “KRISTO NI YOTE” . JINSI YA KUFANYA NOVENA HII: 1.Njoo mbele ya Yesu na umwabudu.(Mbele ya Tabenaklo) 2. Soma Maneno ya Yesu . 3.Soma Maandiko Matakatifu ya tafakari na ujiulize mwenyewe Ni sehemu ipi yenye maana kwangu? Ninajisikiaje ninaposoma? Nitamwambia nini Yesu aliyezungumza nami binafsi kwa njia ya neno? 4. Tumia kiitikio cha sala iliyowekwa. 5.Sali rozari ya Huruma ya Mungu ukitolea nia fulani hasa zile Yesu analeta akilini mwako. . Tumia tafakari ya nyongeza na s...