Posts

Showing posts from January, 2024

SIKU TISA: NOVENA YA MT RITA

Image
  SIKU YA TISA (9) NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA *Kwajina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.* Nina kuja mbele yako, Ee Mtakatifu Rita, siku hii ya mwisho ya Novena hii Takatifu. Ninayasikia mapigo ya moyo katika kipindi hiki kigumu cha maisha yangu yaliyogawanyika. Ninaamini kwamba ombi langu litatimizwa na Bwana kupitia maombezi yako Matakatifu. Lakini ikiwa haiwezekani,ninapaza sauti nikiomba kwanguvu huruma na faraja yako. Usiniache niondoke bila kupata faraja yako. Ee Mtakatifu Rita ,ninaomba unifariji kwa mastahili ya mateso uliyoyapata hapa duniani na katika upweke wako wa sala. Unifariji kwa mastahili ya ukarimu uliokua nao kwa wenye shida unisikilize kwa kwa mastahili ya upendo wako mkuu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa mama yake Bikira Maria Mtakatifu asiye na doa. Kwa mastahili ya ule mwiba Mtakatifu aliokujalia Bwana wetu Yesu Kristo,unisaidie na unifadhili mimi. Hiki ndicho kilio changu cha mwisho kwako wewe mama uliye Mtakatifu wa mambo yaliyoshi...

SIKU NANE: NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

Image
  SIKU YA NANE : NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA *Kwa jina la Baba,na la Mwana, na la Roho Mt. Amina* Ewe kielelezo kitakatifu cha Msalaba Mtukufu, ninapokuona ukiwa umesujudu mbele ya miguu mitakatifu ya Bwana,ninapotafakari paji la uso wako lililojeruhiwa kwa mwiba uliotoka ktk taji la miiba la Yesu Kristo, mchumbawako mpendwa, imani yangu kwako inachanua kwa namna ya ajabu. Wewe ni mtumishi mteule wa Mungu. Mungu amekuzawadia alama ya ufalme wake akakutakatifuza na kukufanya uwe mali yake kabisa. Hivyo sikukosea nilivyoweka imani yangu yote kwako,na nilipojiweka kabisa chini ya ulinzi wako wenye huruma nyingi. Na sasa ni wakati mzuri wa kunisaidia, ukiyajua mahitaji na misaada ninayoomba kutoka kwako. Naamini sala hii kwako wewe mama mpenz sana haitapotea bure. Wewe uliye mfanya miujiza, mfadhili wa mambo ya mbinguni, unayetegemewa na wanadamu wote. Ninakuomba na kukusihi kwa mastahili ya pendo lako kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, uniombee ili nijaliwe haya niombayo( *hapa om...

SIKU YA SABA: NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

Image
SIKU YA SABA(7)   NOVENA YA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA Kwa jina LA Baba, nala Mwana, nala Roho Mtakatifu . AMINA*. Ee mpedwa Rita, ambaye maisha yako yalikuwa yahuzuni. Nielekezee uso wako wa huruma mimi mwenye maumivu makali. Naomba sala zangu, uchovu wangu na kuchechemea kwangu viufikie moyo wako mpole ili uweze kufunguliwa kwangu. Huruma yako ambayo wakati wote uliionesha kwa Jiran, maneno ya aman na faraja, na ushauri Mtakatifu uliowapa watu wote vinivute kukuelekea wewe uliye katika mbingu na unakoishi na kuwa mwombezi wa watu wote waliokata tamaa. Mbele ya miujiza yako mikuu, kifo kinarudi nyuma, vipofu wanapokea nuru, viwete wanasimama, waliopooza wanaponyeshwa na ulemavu wote wa roho na mwili unaondoka kabisa. Je! Nipo peke yangunjsiyefarijiwa na maombezi yako? Sitaamini wala siwezi kuamin hivyo. Nam naamini kwa dhati usimamizi wako na maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ninamatumaini makubwa kuwa nitapata amani, moyoni wang, utulivwana fadhila ninazoomba nitaj...

SIKU YA SITA :NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

Image
 SIKU YA SITA :   NOVENA YA MT.RITA WA KASHIA Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina Nafahamu kuwa sababu ya dhambi zangu sala zangu zimefunikwa na wingu zisiweze kufika katika kiti chako cha enzi. Dhambi zangu ni sababu ya adhabu zangu kubwa. Sina ujasiri wa kuelekeza sauti yangu kwa Yesu. Kwa kuwa mara nyingi sikuthamini huruma yake. Na sasa naiona nguvu yake kuu na ya haki. Mkono wake wa haki umenielekea. Natambua kwamba sistahili baraka za msamaha wake kwani nimegubikwa na huzuni kubwa. Pasipo matumaini ninayalilia madhambi yangu. Niambie Mtakatifu Rita; Je, niendelee kukata tamaa? Hapana. Bwana wetu Yesu Kristo amekuteua kuwa mtetezi wake mwenye nguvu, ili uniombee kwa Yesu wangu aliye juu, msamaha kwa makosa yangu makubwa na nia safi ya kutomtendea dhambi tena. Kwa uamuzi huu thabiti, wa midomo yangu na moyo wangu, nakuelekea wewe. Ee Mtakatifu mtenda miujiza, uniombee kwa Bwana Yesu, fadhila ambazo nazihitaji sana (hapa omba hitaji lako unalotaka ...

SIKU YA TANO:NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

Image
SIKU YA TANO NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA *Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.* *Amina.* *Sala ya Kutubu* Mungu wangu, nimetubu sana niliyokosa kwako. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi. Amina *SALA YA NOVENA* Ewe mchumba mpendwa wa Yesu, Mt. Rita wa Kashia; nakuja kwako tena. Nipo miguuni pako. Navutwa na wema wako kwa roho zenye kutaabika na kusumbuka. Unauona moyo wangu ulivyopondwapondwa kwa magumu ya dunia hii. Sipati tena tabasamu la thamani, roho yangu imevamiwa na mashaka mabaya, imani imetetereka kwa mshituko wa kukata tamaa, kama msituko wa kifo unapiga miayo miguuni pangu. Nielekeze, Ee Mtakatifu mpendwa, nifanye nini katika mazingira haya ya kutisha? Nishauri nimwendee nani katika hali hii ya hatari katika maisha yangu? Kama kweli wewe ni Mtakatifu wa hali zote za kukatisha tamaa, njoo unisaidie kwani najisikia nimepotea. Nakuja kwako wewe ambaye...