Posts

Showing posts from May, 2023

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU.

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU. Bwana Utuhurumie………Utuhurumie! Kristu utuhurumie……..…Utuhurumie! Bwana utuhurumie….. Utuhurumie! Baba mweza wa vyote….. Utuhurumie! Yesu Mwana wa Pekee wa Baba na Mwokozi wa Dunia…….. Utuokoe! Roho wa Baba na Mwana aunganishaye maisha ndani ya Baba na Mwana………Ututakatifuze! Roho Mtakatifu ………. Utusikie! Roho Mtakatifu atokaye kwa Baba na Mwana..... Njoo ndani ya mioyo yetu! Ahadi ya Mungu Baba……Njoo ndani ya mioyo yetu! Mionzi ya Mwanga kutoka Mbinguni……… Njoo ndani ya mioyo yetu! Mwandishi wa vyote vilivyo vizuri……… Njoo ndani ya mioyo yetu! Chanzo cha Maji ya Uzima........ Njoo ndani ya mioyo yetu! Moto utumikao daima... Njoo ndani ya mioyo yetu! Muungano Mtakatifu… Njoo ndani ya mioyo yetu! Roho wa ukweli na upendo... Utuhurumie! Roho wa hekima na elimu... Utuhurumie! Roho wa shauri na nguvu.... Utuhurumie! Roho wa akili na neema ya kumtumikia Mungu…… Utuhurumie! Roho wa neema na sala ........ Utuhurumie! Roho wa amani na subira...... Utuhurumie! Roho wa u...

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TISA, JUMAMOSI

  NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA TISA, JUMAMOSI ROHO MTAKATIFU ANATUPA MAPENDO Maandiko Matakatifu yanatuambia ya kuwa, Roho Mtakatifu, Nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ndiye Upendo katika Baba na Mwana. Upendo hujieneza. Naye Roho Mtakatifu aliye pendo lenyewe la Mungu, hupenda kujieneza na kujishirikisha nasi, na kuwasha ndani yetu moto wa mapendo yake. Roho Mtakatifu ndiye mwenye kutakatifuza roho zetu kwa neema ya utakaso. Neema hiyo ni uzima wa Mungu, ndio huo upendo wa Mungu tunaoshirikishwa. Roho isiyo na neema ya utakaso imetengana na Mungu, haina uzima wake, haina upendo wake, kwa hiyo haiwezi pia kuwa na mapendo ya kweli ya jirani. Ingawa tunaona ishara nyingi za watu kupendana kidugu hapa duniani, mapendo hayo si mapendo ya kweli wala si kamili kama hayatokani na neema ya utakaso rohoni mwa mtu. Kama hakuna neema ya utakaso ndani yetu, Mungu pia hayupo kati yetu. Roho Mtakatifu anatuunganisha na Mungu katika upendo. Pasipo na mapendo hapana mapatano, hapana masi...

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA NANE, IJUMAA

Image
  NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA NANE, IJUMAA ROHO MTAKATIFU ANATUPA MWANGA. Roho Mtakatifu anaangaza akili zetu tuweze kuona ukweli wa Mungu na kuufata. Bila Roho Mtakatifu akili zetu zimo katika giza nene, wala hatuwezi kuona njia ya kutuelekeza kwa Mungu. Mungu alipoumba ulimwengu, dunia ilikuwa giza tupu, haina kitu. Mungu alisema; “Iwe nuru”, ikawa nuru, Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema (Mwa 1;3-4) vivyo hivyo akili ya binadamu bila nuru ya mwanga wa Roho Mtakatifu, ni tupu, ina giza, haiwezi kuona mambo yanayotuelekeza kwa Mungu. Tukiwa na nuru ya Roho Mtakatifu tunaona ukweli wa Mungu jinsi ulivyo. Roho Mtakatifu anapoijia roho ya mtu, anaiangaza akili yake iweze kuona mambo yanayofaa kwa wokovu. Naye akiisha kuiangaza akili ya mtu huimarisha utashi wake na kumwezesha kuchagua daima yaliyo mema. Roho Mtakatifu huiangaza akili iweze kuona ukweli. Kabla ya kuwaaga mitume, Yesu aliwaambia kuwa atawapelekea mfariji mwingine atakayekaa nao siku zote. Roho wa kweli amb...

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA SABA

  NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA SABA, ALHAMISI ROHO MTAKATIFU ANATUPA HEKIMA Hekima tunayopewa na Roho Mtakatifu si sawa kama hekima inayopatikana katika ulimwengu huu. Hekima ya Roho Mtakatifu ni ile Mtk. Paulo aliyowaambia Wakorintho ya kuwa; ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana kama wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu. Lakini, ni kama yasemavyo maandiko; mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao (1Kor 2;8-9). Mtk. Paulo alisema kama vile roho ya mtu ndiyo yenye kufahamu na kutambua yaliyo ndani yake; hivyo pia Roho Mtakatifu ndiye anayefahamu mambo ya Mungu na kutufumbulia sisi mioyoni mwetu. Katika Sikukuu hii ya Pentekoste tunatazamia kumpokea Roho Mtakatifu. Yeye aliye hekima ya Mungu atatufumbulia siri za Mungu na ukweli wake. Ndiye atakayeamsha ndani yetu mapendo ya Yesu Msulibiwa , Mkombozi wetu. Ni yeye atakay...

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA SITA

  NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA SITA, JUMATANO ROHO MTAKATIFU ANATUPA NGUVU “Nitamuomba Baba , naye atawapelekea Mfariji mwingine atakaye kaa nanyi siku zote”. Katika maisha yenu hapa duniani tunahitaji mno kitulizo cha Mungu. Ni jambo la hekima kutafuta kitulizo hicho kwa Mungu wala si kwa viumbe; maana kitulizo kinachopatikana kwa viumbe hapa duniani hakidumu; bali kitulizo kitokacho kwa Mungu ni cha kudumu. Roho Mtakatifu ndio kitulizo chetu cha kweli. Baba ndiye aliyetuumba, Mwana ndiye aliyetukomboa, Roho Mtakatifu ndiye aliyetutakasa mioyo yetu na kutufariji. Kazi ya Roho Mtakatifu sio tu kuwatuliza wale walio na huzuni, bali pia kuwapa moyo wa kuvumilia taabu zozote kwa saburi. Tunahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili tuweze kuishi maisha mema ya kikristu. Katika juhudi zetu za kumtumikia Mungu mara nyingi tunakutana na shida; naye Roho Mtakatifu ndie anayetufariji kwa kutupa nguvu za kupambana na matatizo yote. Maisha yetu hapa duniani yamejaa misalaba. Na misalaba h...

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TANO

  NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA TANO, JUMANNE ROHO MTAKATIFU ANAWATAKASA WAUMINI Walio wa Mungu watafuata yaliyo ya Mungu, na walio wa dunia hufuata yaliyo ya dunia,. Ni mauti kutosheka na mambo yaliyo ya dunia. Uzima na faraja ya kweli hupatikana tu katika mambo ya Mungu. Kwa nguvu zetu sisi wenyewe hatuwezi kutenda lolote jema. Kuweza kwetu kwatoka kwa Mungu, kwatoka kwa Yeye anayetupa kujua, kupenda na kutenda. Mtu anapotenda dhambi, hawezi kuongoka ila kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ndiye anayempa mkosefu neema ya kutambua ubaya wa kosa lakena kuamua kuliacha. Ndiye anayempa pia mkosefu kutambua uzuri wa neema aliyoipoteza na kumrudishia neema hiyo. Ndiye anayempa nguvu za kuidumisha neema hiyo na kuiongeza. Isitoshe, Roho Mtakatifu ndiye anayemuwezesha mtu kuwa na maendeleo katika fadhila na utakatifu. Ndiye anayemjalia imani iliyo msingi wa maisha ya kiKristu. Ndie anayetujalia akili ya kushika mafumbo ya dini yetu na kuishi imani yetu mpaka kufa. Lakini imani peke ya...

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA NNE

  NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA NNE, JUMATATU ROHO MTAKATIFU ANALIUNGANISHA KANISA “Atakapokuja huyu Roho wa kweli , atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yn 16:13) Baada ya kusema hayo, Yesu aliinua macho yake kuelekea mbinguni akasema “Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha kazi uliyonipa niifanye. Naomba ili wote wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba Wewe ulinituma (Yn 17:4,21). Nasi twamuomba Mungu Mwenyezi alijalie kanisa lake umoja wa kweli, awaunganishe wakristu wa madhehebu yote katika zizi moja chini ya mchungaji mmoja. Popote duniani watu wengi, makundi kwa makundi wanavutwa na neema hiyo ya kuungana na kuufikia umoja wa Kanisa. Hata ndugu zetu waliotengana nasi wanazidi kukubali mwongozo wa Roho Mtakatifu na kutaka kurudi katika nyumba ya Baba na kuwa kundi moja chini ya mchungaji mmoja. Isitoshe, hata sasa tena twaweza kuona kwamba kwa namna fulani wamejiunga nasi katika Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kumshuhudia...

NOVENA YA ROHO MTAKATU SIKU YA TATU

  NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA TATU, JUMAPILI ROHO MTAKATIFU ANATUFANYA KUWA MITUME Bwana alisema kwa kinywa cha nabii Yoeli; “Katika siku zile za mwisho asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, waume kwa wake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto….hata watumishi wenu watamiminiwa Roho wangu katika siku zile, nao watautangaza ujumbe wangu. (Mdo.2:17-21) Siku ile ya Pentekoste, bada ya Roho Mtakatifu kulishukia kanisa, mitume waliwakumbusha watu maneno haya ya nabii Yoeli, na miaka mingi baadae, Petro aliwaandikia barua Wakristu wa kwanza akawaambia; kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine, kama vile wakili mwema wa zawadi mbali mbali za Mungu. Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu aliyojaliwa na Mungu ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristu, ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na...

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA PILI

  NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA PILI, JUMAMOSI ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KUENEZA INJILI “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika utawala wa Mungu,” (Yn. 3:5). Kanisa limepewa na Yesu ujumbe wa kuwaletea watu wote uzima mpya, uzima wa Mungu. Yesu aliwaambia mitume wake: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni basi mkawafanye watu wa makabila yote kuwa wafuasi wangu. Wabatizeni kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kuyashika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote mpaka mwisho wa nyakati (Mt.28: 18-20). Sisi tuliobatizwa tumepata kuwa viungo vilivyo hai vya Mwili wa Fumbo wa Kristu; kwa Kipaimara tumeimarishwa na kuthibitishwa na Roho Mtakatifu. Tumekuwa taifa teule. Tumeshirikishwa ule ukuhani wa Kristu. Tumepokea ujumbe wa kueneza utawala wa Mungu. Tunapopokea Sakramenti, na hasa ile Sakmenti ya Ekaristi, tunalisha imani na kuongeza mapendo, ambayo ni msingi wa utume wowote ul...

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA KWANZA

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU  SIKU YA KWANZA, IJUMAA ROHO MTAKATIFU ANATUFARIJI Yesu alipokuwa akiagana na mitume wake, kabla ya kupaa mbinguni, aliwaambia wasiondoke Yerusalemu mpaka hapo watakapokuwa wamempokea Roho Mtakatifu. Aliwaambia: “Wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni, mtajazwa nguvu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yuda na Samaria, hata kwenye mipaka yote ya dunia.” (Mdo.1:8) Waliendelea kusali pamoja toka hapo Yesu alipopaa mbinguni mpaka siku ya Pentekoste. Waliomba Roho Mtakatifu awashukie, awajaze na mapaji yake. Na baada ya siku tisa Roho Mtakatifu aliwashukia hao kundi dogo nao wakawa chanzo cha Kanisa lililopata kuenea duniani kote. Siku hizo tisa za kusali zinaitwa NOVENA; na kila mwaka wakati huu, wakristu wakifuata mfano wa mitume, wanasali muda wa siku tisa kabla ya Sikukuu ya Pentekoste. Wanamuomba Roho Mtakatifu awashukie, awajaze nguvu na wingi wa mapaji yake. Wakati huu wa NOVENA , Tunayo mengi ya kuliombea Kanisa na ...