LITANIA YA ROHO MTAKATIFU.

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU.


Bwana Utuhurumie………Utuhurumie!
Kristu utuhurumie……..…Utuhurumie!
Bwana utuhurumie….. Utuhurumie!
Baba mweza wa vyote….. Utuhurumie!
Yesu Mwana wa Pekee wa Baba na Mwokozi wa Dunia…….. Utuokoe!
Roho wa Baba na Mwana aunganishaye maisha ndani ya Baba na Mwana………Ututakatifuze!
Roho Mtakatifu ………. Utusikie!
Roho Mtakatifu atokaye kwa Baba na Mwana..... Njoo ndani ya mioyo yetu!
Ahadi ya Mungu Baba……Njoo ndani ya mioyo yetu!
Mionzi ya Mwanga kutoka Mbinguni……… Njoo ndani ya mioyo yetu!
Mwandishi wa vyote vilivyo vizuri………
Njoo ndani ya mioyo yetu!
Chanzo cha Maji ya Uzima........
Njoo ndani ya mioyo yetu!
Moto utumikao daima... Njoo ndani ya mioyo yetu!
Muungano Mtakatifu… Njoo ndani ya mioyo yetu!
Roho wa ukweli na upendo... Utuhurumie!
Roho wa hekima na elimu... Utuhurumie!
Roho wa shauri na nguvu.... Utuhurumie!
Roho wa akili na neema ya kumtumikia Mungu…… Utuhurumie!
Roho wa neema na sala ........ Utuhurumie!
Roho wa amani na subira...... Utuhurumie!
Roho wa usafi na uaminifu.... Utuhurumie!
Kitulizo cha Roho…………Utuhurumie!
Roho aletaye Utakatifu…Utuhurumie!
Roho uongozaye Kanisa.. Utuhurumie!
Zawadi kutoka kwa Mungu juu Mbinguni……Utuhurumie!
Roho ajazaye ulimwengu...... Utuhurumie!
Roho Mtakatifu.........
Tupe neema ya kuchukia dhambi!
Roho Mtakatifu……….. njoo ufanye upya sura ya ulimwengu!
Roho Mtakatifu……….. Jaza roho zetu kwa mwanga wako!
Roho Mtakatifu………… Ifuraishe mioyo yetu kwa sheria yako!
Roho Mtakatifu….....
Washa moto wa mapendo ndani yetu! Roho Mtakatifu………… Jaza mioyo yetu na hazina ya neema yako!
Roho Mtakatifu…….... Tufundishe kusali vyema!
Roho Mtakatifu………… Tuangaze kwa nguvu zako za Ki-Mungu zitupatiazo moyo wa kutenda daima yaliyo mema!
Roho Mtakatifu……………… Tuongoze Kwenye njia ya wokovu!
Roho Mtakatifu…………… Tuweze kufahamu yale ya muhimu tu!
Roho Mtakatifu…………… Tupe hamu ya kuitafuta fadhila yako!
Roho Mtakatifu……………… Tusaidie tuweze Kupata fadhila zote!
Roho Mtakatifu…………… Tupe uvumilivu tuweze kutenda yaliyo mema tu!
Roho Mtakatifu……………
Tunaomba uwe zawadi ya uzima wetu!

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia………
Tushushie Roho wako Mtakatifu!
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia…………
Jaza mioyo yetu kwa mapaji yako ya Roho Mtakatifu!
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia…………
Tupe roho ya hekima na neema ya kumsifu Mungu.

(W)..... Njoo Roho Mtakatifu uzijaze roho za waumini wako uwashe moto wa mapendo yako ndani ya mioyo yetu

TUOMBE
Ee Mungu Baba mwenye huruma tujalie Roho wako alete Mwanga kwetu ili apate kututakasa na kuingiza ndani ya mioyo yetu Baraka za kuweza kutenda yale yaliyo mema.
Tunaomba hayo kupitia kwa Mwanao Mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo, anbaye anaishi na kutawala pamoja nawe katika Umoja wa Roho Mtakatifu.
AMINA

Atukuzwe Baba…..x3

Comments

Popular posts from this blog

SIKU NANE: NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

SIKU YA SABA: NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA