SIKU NANE: NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

 SIKU YA NANE:

NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA

*Kwa jina la Baba,na la Mwana, na la Roho Mt. Amina*
Ewe kielelezo kitakatifu cha Msalaba Mtukufu, ninapokuona ukiwa umesujudu mbele ya miguu mitakatifu ya Bwana,ninapotafakari paji la uso wako lililojeruhiwa kwa mwiba uliotoka ktk taji la miiba la Yesu Kristo, mchumbawako mpendwa, imani yangu kwako inachanua kwa namna ya ajabu. Wewe ni mtumishi mteule wa Mungu. Mungu amekuzawadia alama ya ufalme wake akakutakatifuza na kukufanya uwe mali yake kabisa.
🛐Hivyo sikukosea nilivyoweka imani yangu yote kwako,na nilipojiweka kabisa chini ya ulinzi wako wenye huruma nyingi. Na sasa ni wakati mzuri wa kunisaidia, ukiyajua mahitaji na misaada ninayoomba kutoka kwako. Naamini sala hii kwako wewe mama mpenz sana haitapotea bure.
🛐Wewe uliye mfanya miujiza, mfadhili wa mambo ya mbinguni, unayetegemewa na wanadamu wote. Ninakuomba na kukusihi kwa mastahili ya pendo lako kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, uniombee ili nijaliwe haya niombayo( *hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Ritha*. )
🛐Mungu hakukatalii wew kitu chochote; kwa maombezi yako,miujiza hufanywa,neema na fadhila maalumu hupatikana. Hivyo, kwa moyo wangu wote na matumaini ya dhati,ninasubiri nikitegemea kupata haya niliyoomba kwa Bwana Mungu.
*Baba Yetu x3,
Salamu Maria x3
na Akukuzwe Baba x3*
✝Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke .
*Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete:- watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
🛐Kwa maombezi yako: radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka_ .
*Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete:- watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
🛐Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako
*Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi:- watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
🛐Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele.
*Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete:- watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.*
*KIONGOZI* : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Ritha.
*WOTE:* Kwa muhuri wa upendo na mateso.
*TUOMBE;* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele . AMINA
🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐
*LITANIA KWA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA*
-----------------------------------
Bwana Utuhurumie,
Kristo Utuhurumie,
Bwana Utuhurumie,
-----------------------------------
*Kiitikio *"Utuhurumie"*
Baba wa Mbinguni, Mungu,
Mwana Mkombozi wa Dunia,Mungu,
Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja,
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Maria Imakulata Mama wa Mungu
Maria, Mama mfariji wa wanaoteseka
Maria, Malkia wa Watakatifu wote
Maria, Mwombezi mpenzi wa Mt Rita
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Mt Rita, Zawadi toka Mbinguni:
Mt Rita, Mwombezi wetu mwenye nguvu:
Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu:
Mt Rita, mstaajabiwa tangu utoto wako:
Mt Rita, mpenda upweke:
Mt Rita, Kielelezo cha usafi wa moyo:
Mt Rita, kielelezo cha upole wote:
Mt Rita, kielelezo cha mke mwema:
Mt Rita, kielelezo bora cha mama mtaratibu:
Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli:
Mt Rita, kielelezo hai cha kujikatalia:
Mt Rita, kioo cha maisha ya kitawa:
Mt Rita, kioo cha utii;
Mt Rita, mvumilivu wa kustajabiwa;
Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka;
Mt Rita, shahidi katika kufanya toba
Mt Rita, mjane mtakatifu;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkereketwa wa kuitikia wito mtakatifu;
Mt Rita, aliyeingizwa utawani kimuujiza;
Mt Rita, harufu nzuri ya manemane;
Mt Rita, bustani ya kila fadhila;
Mt Rita, mpendezwa na Yesu Msulubiwa;
Mt Rita, uliyechomwa na mwiba kwenye paji la uso;
Mt Rita, binti mpendevu wa Bikira Maria;
Mt Rita, mwenye kiu ya upendo wa Kimungu;
Mt Rita, uliyevikwa utukufu;
Mt Rita, lulu ya mbinguni;
Mt Rita, utukufu wa shirika la Mt Augustino;
Mt Rita, tunu ya thamani ya Umbria;
Mt Rita, mwenye nguvu za utakatifu;
Mt Rita, msamaha wa wanaopata mahangaiko;
Mt Rita, mfariji wa wanaoteseka;
Mt Rita, nanga ya wokovu;
Mt Rita, mwombezi wa wagonjwa;
Mt Rita, mwombezi wa mambo yaliyoshindikana;
Mt Rita, kimbilio la walio hatarini;
Mt Rita, msaada wenye nguvu kwa wote;
Mt Rita, mastaajabio ya ulimwengu;
Mt Rita, uliyepokewa mbinguni kwa furaha;
-----------------------------------
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusamehe Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusikilize Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia *"Utuhurumie"*
----------------------------------
*K:* Umemtia alama Ee Bwana mtumishi wako Rita
*W:* Kwa mhuli wa upendo na mateso
*TUOMBE*:
Ee Mungu , ambaye katika wema wako wa daima, umependa kusikiliza maombezi ya mtumishi wako Rita. Utujalie kupitia maombezi yake, yale ambayo yameshindikana kwa nguvu za kibinadamu. Utuhurumie sisi tunaoteseka, uwasaidie wote wasiokuamini wajue kuwa wewe ni tuzo la wanyenyekevu, mfariji wa wote wenye hofu, na nguvu ya wanyonge. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
------------------------------------
🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐🛐
*Kila baada ya kusali novena ya siku , tunasali litania hii kwa siku zote 12*

Comments

Popular posts from this blog

SIKU YA SABA: NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA