SIKU TISA: NOVENA YA MT RITA
SIKU YA TISA (9)
NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA
*Kwajina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*
Nina kuja mbele yako, Ee Mtakatifu Rita, siku hii ya mwisho ya Novena hii Takatifu. Ninayasikia mapigo ya moyo katika kipindi hiki kigumu cha maisha yangu yaliyogawanyika. Ninaamini kwamba ombi langu litatimizwa na Bwana kupitia maombezi yako Matakatifu. Lakini ikiwa haiwezekani,ninapaza sauti nikiomba kwanguvu huruma na faraja yako. Usiniache niondoke bila kupata faraja yako.
Ee Mtakatifu Rita ,ninaomba unifariji kwa mastahili ya mateso uliyoyapata hapa duniani na katika upweke wako wa sala. Unifariji kwa mastahili ya ukarimu uliokua nao kwa wenye shida unisikilize kwa kwa mastahili ya upendo wako mkuu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa mama yake Bikira Maria Mtakatifu asiye na doa. Kwa mastahili ya ule mwiba Mtakatifu aliokujalia Bwana wetu Yesu Kristo,unisaidie na unifadhili mimi.
Hiki ndicho kilio changu cha mwisho kwako wewe mama uliye Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa. Ninakuomba ujidhihirishe katika mwanga wako halisi, ili Mungu anijalie haya ninayo yaomba.
*(hapa omba hitaji lako unalotaka kumuomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita)*
Kwa msaada wako ninadhamiria kuachana na mwenendo wangu potofu, ili niwe muenezaji wa nguvu za Mungu na uzuri wa mambo ya Mbinguni. Ninaahidi pia mahali pako pa upweke, Ee Mtakatifu wa sala,huko Kashia,na au kwenye sanamu yako: ili niweze kuungana nawe katika kuabudu na kushukuru kwa fadhila za Mbinguni nilizozipata kwa maombezi yako kutoka kwa Mwokozi wetu Azizi Yesu Kristo.
*Baba Yetu 3, Salamu Maria 3, Atukuzwe 3*
*KIONGOZI* : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
*WOTE* :Kwa mhuri wa upendo na mateso.
*TUOMBE* : Ee Mungu,uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka . Unayeishi na kutawala, daima na milele. *Amina*
Comments
Post a Comment