SIKU YA SITA :NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA
SIKU YA SITA :
NOVENA YA MT.RITA WA KASHIA
Nafahamu kuwa sababu ya dhambi zangu sala zangu zimefunikwa na wingu zisiweze kufika katika kiti chako cha enzi.
Dhambi zangu ni sababu ya adhabu zangu kubwa. Sina ujasiri wa kuelekeza sauti yangu kwa Yesu. Kwa kuwa mara nyingi sikuthamini huruma yake. Na sasa naiona nguvu yake kuu na ya haki. Mkono wake wa haki umenielekea.
Natambua kwamba sistahili baraka za msamaha wake kwani nimegubikwa na huzuni kubwa. Pasipo matumaini ninayalilia madhambi yangu. Niambie Mtakatifu Rita; Je, niendelee kukata tamaa? Hapana. Bwana wetu Yesu Kristo amekuteua kuwa mtetezi wake mwenye nguvu, ili uniombee kwa Yesu wangu aliye juu, msamaha kwa makosa yangu makubwa na nia safi ya kutomtendea dhambi tena.
Kwa uamuzi huu thabiti, wa midomo yangu na moyo wangu, nakuelekea wewe. Ee Mtakatifu mtenda miujiza, uniombee kwa Bwana Yesu, fadhila ambazo nazihitaji sana (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Katika muda huu wa uchovu mkubwa, huzuni na kuachwa pweke; Ee Rita, neno lako kwa Yesu litafungua huruma na msamaha wake. Sema neno na Yesu atakusikia.
Baba Yetu (3), Salamu Maria (3) na Atukuzwe Baba (3).
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.…..
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.…..
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele.
Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete.…..
Kiongozi: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE:
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
*LITANIA KWA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA*
-----------------------------------
Bwana Utuhurumie,
Kristo Utuhurumie,
Bwana Utuhurumie,
-----------------------------------
*Kiitikio *"Utuhurumie"*
Baba wa Mbinguni, Mungu,
Mwana Mkombozi wa Dunia,Mungu,
Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja,
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Maria Imakulata Mama wa Mungu
Maria, Mama mfariji wa wanaoteseka
Maria, Malkia wa Watakatifu wote
Maria, Mwombezi mpenzi wa Mt Rita
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Mt Rita, Zawadi toka Mbinguni:
Mt Rita, Mwombezi wetu mwenye nguvu:
Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu:
Mt Rita, mstaajabiwa tangu utoto wako:
Mt Rita, mpenda upweke:
Mt Rita, Kielelezo cha usafi wa moyo:
Mt Rita, kielelezo cha upole wote:
Mt Rita, kielelezo cha mke mwema:
Mt Rita, kielelezo bora cha mama mtaratibu:
Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli:
Mt Rita, kielelezo hai cha kujikatalia:
Mt Rita, kioo cha maisha ya kitawa:
Mt Rita, kioo cha utii;
Mt Rita, mvumilivu wa kustajabiwa;
Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka;
Mt Rita, shahidi katika kufanya toba
Mt Rita, mjane mtakatifu;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkereketwa wa kuitikia wito mtakatifu;
Mt Rita, aliyeingizwa utawani kimuujiza;
Mt Rita, harufu nzuri ya manemane;
Mt Rita, bustani ya kila fadhila;
Mt Rita, mpendezwa na Yesu Msulubiwa;
Mt Rita, uliyechomwa na mwiba kwenye paji la uso;
Mt Rita, binti mpendevu wa Bikira Maria;
Mt Rita, mwenye kiu ya upendo wa Kimungu;
Mt Rita, uliyevikwa utukufu;
Mt Rita, lulu ya mbinguni;
Mt Rita, utukufu wa shirika la Mt Augustino;
Mt Rita, tunu ya thamani ya Umbria;
Mt Rita, mwenye nguvu za utakatifu;
Mt Rita, msamaha wa wanaopata mahangaiko;
Mt Rita, mfariji wa wanaoteseka;
Mt Rita, nanga ya wokovu;
Mt Rita, mwombezi wa wagonjwa;
Mt Rita, mwombezi wa mambo yaliyoshindikana;
Mt Rita, kimbilio la walio hatarini;
Mt Rita, msaada wenye nguvu kwa wote;
Mt Rita, mastaajabio ya ulimwengu;
Mt Rita, uliyepokewa mbinguni kwa furaha;
-----------------------------------
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusamehe Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusikilize Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia *"Utuhurumie"*
----------------------------------
*K:* Umemtia alama Ee Bwana mtumishi wako Rita
*W:* Kwa mhuli wa upendo na mateso
*TUOMBE*:
Ee Mungu , ambaye katika wema wako wa daima, umependa kusikiliza maombezi ya mtumishi wako Rita. Utujalie kupitia maombezi yake, yale ambayo yameshindikana kwa nguvu za kibinadamu. Utuhurumie sisi tunaoteseka, uwasaidie wote wasiokuamini wajue kuwa wewe ni tuzo la wanyenyekevu, mfariji wa wote wenye hofu, na nguvu ya wanyonge. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
------------------------------------
*Kila baada ya kusali novena ya siku , tunasali litania hii kwa siku zote 12*
Comments
Post a Comment