SIKU YA TANO:NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA
SIKU YA TANO
NOVENA YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA
*Sala ya Kutubu*
Mungu wangu, nimetubu sana
niliyokosa kwako. Kwani ndiwe
mwema, ndiwe mwenye
kupendeza. Wachukizwa na
dhambi, basi sitaki kukosa
tena. Nitafanya kitubio,
naomba neema yako nipate
kurudi. Amina
*SALA YA NOVENA*
Ewe mchumba mpendwa wa Yesu, Mt. Rita wa Kashia; nakuja kwako tena. Nipo miguuni pako. Navutwa na wema wako kwa roho zenye kutaabika na kusumbuka. Unauona moyo wangu ulivyopondwapondwa kwa magumu ya dunia hii. Sipati tena tabasamu la thamani, roho yangu imevamiwa na mashaka mabaya, imani imetetereka kwa mshituko wa kukata tamaa, kama msituko wa kifo unapiga miayo miguuni pangu. Nielekeze, Ee Mtakatifu mpendwa, nifanye nini katika mazingira haya ya kutisha? Nishauri nimwendee nani katika hali hii ya hatari katika maisha yangu?
Kama kweli wewe ni Mtakatifu wa hali zote za kukatisha tamaa, njoo unisaidie kwani najisikia nimepotea. Nakuja kwako wewe ambaye kila mara wawahurumia wanaoteseka. Nakuja kwako unisaidie. Je, hutanionea huruma kutokana na hali yangu? Mtakatifu Rita najua u mwema sana. Najua hivyo, ndiyo maana najiweka mikononi mwako kwa moyo wangu wote ili unijibu kwa njia ya Yesu, lile ombi langu ambalo kwa imani kubwa naliomba ( *Taja ombi lako)*
*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba ( 3)* ..
+ Kwa njia ya Mt. Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na* **wafu wanarudishiwa uhai.*
+ Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. *Unawasaidia vipofu**.....*
+ Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu* ....
+ Kwa Mungu Mtakatifu na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia Vipofu* ...
K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso.
Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidi kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina
Atukuzwe Baba..
Mt. Rita wa Kashia, Utuombee ( mara tatu)
*Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu* . *Amina.*
*LITANIA KWA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA*
-----------------------------------
Bwana Utuhurumie,
Kristo Utuhurumie,
Bwana Utuhurumie,
-----------------------------------
*Kiitikio *"Utuhurumie"*
Baba wa Mbinguni, Mungu,
Mwana Mkombozi wa Dunia,Mungu,
Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja,
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Maria Imakulata Mama wa Mungu
Maria, Mama mfariji wa wanaoteseka
Maria, Malkia wa Watakatifu wote
Maria, Mwombezi mpenzi wa Mt Rita
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Mt Rita, Zawadi toka Mbinguni:
Mt Rita, Mwombezi wetu mwenye nguvu:
Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu:
Mt Rita, mstaajabiwa tangu utoto wako:
Mt Rita, mpenda upweke:
Mt Rita, Kielelezo cha usafi wa moyo:
Mt Rita, kielelezo cha upole wote:
Mt Rita, kielelezo cha mke mwema:
Mt Rita, kielelezo bora cha mama mtaratibu:
Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli:
Mt Rita, kielelezo hai cha kujikatalia:
Mt Rita, kioo cha maisha ya kitawa:
Mt Rita, kioo cha utii;
Mt Rita, mvumilivu wa kustajabiwa;
Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka;
Mt Rita, shahidi katika kufanya toba
Mt Rita, mjane mtakatifu;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkereketwa wa kuitikia wito mtakatifu;
Mt Rita, aliyeingizwa utawani kimuujiza;
Mt Rita, harufu nzuri ya manemane;
Mt Rita, bustani ya kila fadhila;
Mt Rita, mpendezwa na Yesu Msulubiwa;
Mt Rita, uliyechomwa na mwiba kwenye paji la uso;
Mt Rita, binti mpendevu wa Bikira Maria;
Mt Rita, mwenye kiu ya upendo wa Kimungu;
Mt Rita, uliyevikwa utukufu;
Mt Rita, lulu ya mbinguni;
Mt Rita, utukufu wa shirika la Mt Augustino;
Mt Rita, tunu ya thamani ya Umbria;
Mt Rita, mwenye nguvu za utakatifu;
Mt Rita, msamaha wa wanaopata mahangaiko;
Mt Rita, mfariji wa wanaoteseka;
Mt Rita, nanga ya wokovu;
Mt Rita, mwombezi wa wagonjwa;
Mt Rita, mwombezi wa mambo yaliyoshindikana;
Mt Rita, kimbilio la walio hatarini;
Mt Rita, msaada wenye nguvu kwa wote;
Mt Rita, mastaajabio ya ulimwengu;
Mt Rita, uliyepokewa mbinguni kwa furaha;
-----------------------------------
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusamehe Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusikilize Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia *"Utuhurumie"*
----------------------------------
*K:* Umemtia alama Ee Bwana mtumishi wako Rita
*W:* Kwa mhuli wa upendo na mateso
*TUOMBE*:
Ee Mungu , ambaye katika wema wako wa daima, umependa kusikiliza maombezi ya mtumishi wako Rita. Utujalie kupitia maombezi yake, yale ambayo yameshindikana kwa nguvu za kibinadamu. Utuhurumie sisi tunaoteseka, uwasaidie wote wasiokuamini wajue kuwa wewe ni tuzo la wanyenyekevu, mfariji wa wote wenye hofu, na nguvu ya wanyonge. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
------------------------------------
*Kila baada ya kusali novena ya siku , tunasali litania hii kwa siku zote 12*
Comments
Post a Comment