SIKU YA TATU -NOVENA YA MT RITA WA KASHIA
NOVENA YA MT.RITA WA KASHIA SIKU YA TATU
kwa jina la Baba,na la Mwana,na la Roho Mtakatifu.Amina
Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa mapumziko,huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu.Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu,najiona nimepotea kabisa.Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Ritha,unaye ng'ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usio kifani katika nguvu na nguzo za kanisa katoliki,natambua wewe unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu.Ninakuamini,kwa hamu nangojea,kupata kile nikiombacho (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungi kupitia Mtakatifu Ritha)
◇ Nifikshie ombi langu kwa Yesu wa msalaba.Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopata majaribu,kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako.Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu.Kwa sadaka yako ya kishujaa,uliyomtolea Mungu wana wako,ukiomba wasinajisiwe kwa dhambi.Uniombee kwa Mungu.Hicho ni kifo dinicha moyo wako.Kupitia mateso ambayo Bwana Yesu kristo aliruhusu yakupate ili utakaswe katika majonzi yako,kwa njia ya majiribu mengi yaliyokupata na sadaka nyingi ulizotoa,uniombee ili nijaliwe kupewa ombi langu ninalongojea kwa hamu.
Baba Yetu(3),salamu maria(3)na atukuzwe Baba(3)
◇kwa njia ya Mtakatifu Ritha ;homa,madonda na tauni ,viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
◇kwa maombezi yako;radi,tetemeko la ardhina moto havina nguvu.kwa utakatifu wako mitego yote,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
◇Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana.Watu wengi wanaimba sifa zako.Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
◇Kwa Mungu Mtakatifu,na kwa mwanae ziwe sifa,utukufu na heshima,sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
kiongozi: umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
wote:kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE Ee Mungu uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Ritja kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso.Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya metso yako,ili tupate tuzo uliotuhadia kwa wapole na wanaoteseka.Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
*LITANIA KWA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA*
-----------------------------------
Bwana Utuhurumie,
Kristo Utuhurumie,
Bwana Utuhurumie,
-----------------------------------
*Kiitikio *"Utuhurumie"*
Baba wa Mbinguni, Mungu,
Mwana Mkombozi wa Dunia,Mungu,
Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu, Mungu Mmoja,
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Maria Imakulata Mama wa Mungu
Maria, Mama mfariji wa wanaoteseka
Maria, Malkia wa Watakatifu wote
Maria, Mwombezi mpenzi wa Mt Rita
-----------------------------------
*Kiitikio* “Utuombee"*
Mt Rita, Zawadi toka Mbinguni:
Mt Rita, Mwombezi wetu mwenye nguvu:
Mt Rita, uliyejaliwa Utukufu:
Mt Rita, mstaajabiwa tangu utoto wako:
Mt Rita, mpenda upweke:
Mt Rita, Kielelezo cha usafi wa moyo:
Mt Rita, kielelezo cha upole wote:
Mt Rita, kielelezo cha mke mwema:
Mt Rita, kielelezo bora cha mama mtaratibu:
Mt Rita, kielelezo cha msamaha wa kweli:
Mt Rita, kielelezo hai cha kujikatalia:
Mt Rita, kioo cha maisha ya kitawa:
Mt Rita, kioo cha utii;
Mt Rita, mvumilivu wa kustajabiwa;
Mt Rita, shujaa wa kujitoa sadaka;
Mt Rita, shahidi katika kufanya toba
Mt Rita, mjane mtakatifu;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkarimu kwa masikini;
Mt Rita, mkereketwa wa kuitikia wito mtakatifu;
Mt Rita, aliyeingizwa utawani kimuujiza;
Mt Rita, harufu nzuri ya manemane;
Mt Rita, bustani ya kila fadhila;
Mt Rita, mpendezwa na Yesu Msulubiwa;
Mt Rita, uliyechomwa na mwiba kwenye paji la uso;
Mt Rita, binti mpendevu wa Bikira Maria;
Mt Rita, mwenye kiu ya upendo wa Kimungu;
Mt Rita, uliyevikwa utukufu;
Mt Rita, lulu ya mbinguni;
Mt Rita, utukufu wa shirika la Mt Augustino;
Mt Rita, tunu ya thamani ya Umbria;
Mt Rita, mwenye nguvu za utakatifu;
Mt Rita, msamaha wa wanaopata mahangaiko;
Mt Rita, mfariji wa wanaoteseka;
Mt Rita, nanga ya wokovu;
Mt Rita, mwombezi wa wagonjwa;
Mt Rita, mwombezi wa mambo yaliyoshindikana;
Mt Rita, kimbilio la walio hatarini;
Mt Rita, msaada wenye nguvu kwa wote;
Mt Rita, mastaajabio ya ulimwengu;
Mt Rita, uliyepokewa mbinguni kwa furaha;
-----------------------------------
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusamehe Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia, *"Utusikilize Bwana"*
Mwanakondoo wa Mungu uondoae dhambi za dunia *"Utuhurumie"*
----------------------------------
*K:* Umemtia alama Ee Bwana mtumishi wako Rita
*W:* Kwa mhuli wa upendo na mateso
*TUOMBE*:
Ee Mungu , ambaye katika wema wako wa daima, umependa kusikiliza maombezi ya mtumishi wako Rita. Utujalie kupitia maombezi yake, yale ambayo yameshindikana kwa nguvu za kibinadamu. Utuhurumie sisi tunaoteseka, uwasaidie wote wasiokuamini wajue kuwa wewe ni tuzo la wanyenyekevu, mfariji wa wote wenye hofu, na nguvu ya wanyonge. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina
*Kila baada ya kusali novena ya siku , tunasali litania hii kwa siku zote 12*
Comments
Post a Comment